Friday, April 26, 2013

Mechi ya Simba yahairishwa kupisha muungano

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa ichezwe Aprili 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa itafanyika Mei 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo. Mabadiliko hayo yametokana na Serikali kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano ambazo kitaifa zitafanyika kesho (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi washabiki kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo na ghafla. Ratiba ya mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo.

No comments:

Post a Comment