Timu ya Azam FC leo imetoka droo ya goli 1-1 na Coast Union ya Tanga katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliofanyika jijini Tanga. Kwa matokeo haya Azam FC imefikisha pointi 48 na kuitangazia rasmi timu ya Yanga kuwa mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara mwaka 2012/13. Yanga kwa sasa ina pointi 56 na imebakiza michezo miwili, kwa pointi hizo 56 hakuna timu yoyote kwenye ligi ambayo inaweza kuzifikisha na hivyo kuitangaza Yanga kuwa mabingwa. Yanga imebakiza michezo miwili dhidi ya Coast Union na Simba michezo itakayofanyika mwezi ujao. Yanga kama mabingwa wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya mabingwa barani Afrika na Azam FC wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya washindi barani Afrika msimu ujao. Azam wanatarijiwa kuondoka jumapili hii April 28 kuelekea Morocco ambapo itacheza na AS FAR katika mchezo wa marudiano kombe la washindi barani Afrika baada ya mchezo wa kwanza kutoka droo ya bila kufungana kwenye mchezo uliofanyika jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment