Baba mzazi wa mshambuliaji wa Santos Neyamar amedhibitisha
kuwa mchezaji huyo atahamia Ulaya baada ya kombe la dunia mwakani. Baba Neymar
alisema ‘ Mtoto wangu yupo tayari kuondoka Santos, ila hawezi kuondoka hadi
fainali za kombe la dunia ziishe, lakini hadi sasa hivi nafikiria Barcelona
ndiyo timu atakayoweza kwenda kwasababu ya mahusiano mazuri yaliyopo kati ya
Santos na Barca. Naye wakala wa Barcelona ambaye yupo Brazil kufuatilia
uhamisho wa Neymar bwana Andre Cury amesema Barcelona ipo tayari wakati wowote
kumsajili Neymar kwa kiasi cha fedha Santos watakachohitaji, ila hadi sasa
Barcelona wapo tayari kutoa paundi milioni 50 kwa ajili ya kumnasa Neymar ikiwa
ni kiasi hicho hicho ambacho Real Madrid wametangaza pia kukitoa.
Neymar
mchezaji anayesemekana kuja kuwa mchezaji bora barani Ulaya na Duniani baada ya
kuonesha kiwango cha juu akiwa na umri mdogo wa miaka 21 ameshakuwa mchezaji
bora wa bara la Amerika ya kusini, ameshashinda kikombe cha goli bora la FIFA
mwaka 2011 na alishakuwa kwenye kinyang’anyiro cha kumchagua mchezaji bora wa
dunia akiwa na umri wa miaka 20 na 21, mbali na hayo ameshacheza mechi 32
kwenye timu ya taifa na kufunga magoli 20 na vilevile Neyam ndiye mchezaji
tegemeo kwa Brazil kwenye kombe la dunia mwakani.
No comments:
Post a Comment