Wednesday, April 24, 2013

Huu ni uchokozi ama???

Cab
Katika kusherekea ushindi wa ligi kuu nchini Uingereza wachezaji wa Man utd walifanya kituko jijini Manchester baada ya kupanda teksi iliyobandikwa matangazo ya Man city ambao ni timu pinzani mkubwa wa Man utd. Wachezaji hao Nemanja Vidic, Rio Ferdinand na Anderson walipanda teksi hiyo walipokuwa wanaelekea kwenye bar ya Sakura iliyopo jirani na Old Traford kukutana na wenzao waliokusanyika kusherekea ushindi. Dereva wa teksi hiyo alipoulizwa kwanini wachezaji hao walipanda alisema ' nadhani walikuwa wanatania wapinzani wao, lakini pia ni teksi ambayo wamezoea kuiona maana ni teksi hii moja tu iliyobandikwa matangazo ya Man city'. 

No comments:

Post a Comment