Magoli yaliyofungwa na Lewandowski katika dakika ya 8, 50, 55 na 66 yameizamisha Real Madrid goli nne kwa moja dhidi ya Dortmund katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya UEFA champions. Matokeo haya ni picha tosha kuwa timu za Ujerumani zitatakutana Wembley katika fainali licha ya kuwa waswahili wanasema mpira unadunda. Ni miujiza pekee ndiyo imebakia kwa timu za Hispania Real Madrid na Barcelona kuingia fainali ya UEFA champions. Mechi za marudiano zitafanyika wiki ijayo tarehe 30 April na 1 May. Katika mchezo huu Dortmund waliwakilishwa na Weidenfeller, Subotic, Hummels, Piszczek (Grosskreutz 82) , Schmelzer, Bender, Gundogan (Schieber 90), Reus, Gotze, Lewandowski, Blaszczykowski (Kehl 82) Real Madrid Diego López, Varane, Pepe, Sergio Ramos, Coentrão, Khedira, Ronaldo, Özil, Xabi Alonso (Kaka 80), Modric (Di Maria 68), Higuaín (Benzema 69)
Subs: Casillas, Albiol, Callejon, Nacho.
No comments:
Post a Comment