Ni kawaida kila wiki UEFA kutangaza kikosi bora ambacho kinajumuisha wachezaji mbalimbali kutoka kwenye vilabu tofauti barani Ulaya. Lakini kikosi cha wiki hii kimedhihirisha wazi uwezo wa timu za Ujerumani zilizoonesha kiwango cha hali ya juu wiki hii baada ya kushinda kwa idadi kubwa ya magoli dhidi ya timu za Hispania nchini ambayo ni ya kwanza kwenye viwango vya FIFA duniani. Katika mechi za nusu fainali wiki hii Bayern ilishinda magoli manne kwa bila dhid ya Barcelona na Dortmund walishinda magoli manne kwa moja dhidi ya Madrid. Ifuatayo ni kumi na moja bora ya UEFA wiki hii.
No comments:
Post a Comment