Baada ya Lewandowski kupachika goli nne kwenye mechi ya nusu
fainali kati ya Dortmund na Real Madrid, kocha wa Man utd Sir Alex amezidi
kuvutiwa na mchezaji huyo kiasi cha kutenga bajeti ya paundi milioni 30 ili
kumnasa mshambuliaji huyo wa Borussia Dortmund. Hadi jumatano ya wiki hii Man utd ilikuwa bado
haijaridhishwa kwa asimilia mia moja na kiwango cha Lewandowski kiasi cha kumtuma
mshauri mmoja wa Sir Alex kwenda Ujerumani kumwangalia mchezaji huyo akicheza
mechi dhidi ya Real Madrid, lakini baada ya mechi hiyo ripoti ya mshauri wa Sir
Alex ilionesha kuridhishwa na kiwango cha mchezaji huyo kiasi cha kumwekea bajeti
ya paundi mil 30 ili kumsajili Lewandowski akiwa ndiyo chaguo namba moja la Ferguson katika msimu ujao wa usajili.
Mbali ya United, PSG na Bayern Munich pia zimekuwa zikimuwinda mshambuliaji huyo
kwa karibu zaidi ili kuimarisha vikosi vyao ila Man utd na Bayern ndiyo timu zilizopo kwenye nafasi nzuri kumnasa Lewandowski zaidi ya PSG timu ambayo bado hajavutiwa nayo. Lewandowski hadi sasa ameshacheza
mechi 9 kwenye michuano ya UEFA na kufunga magoli 10 wakati kwenye ligi ya
Ujerumani anaongoza kwa ufungaji wa magoli 23 hadi sasa.
No comments:
Post a Comment