Wilshere, Walcott na Cazorla (WWC) wametajwa kuwa wachezaji muhimu
sana kwa Arsenal. Wachezaji hawa wanacheza nafasi ya kiungo na ushambuliaji
wamekuwa ni chachu kubwa ya ushindi kwenye timu ya Arsenal. Arteta ni mchezaji
mzuri na ana uwezo mzuri wa kumili na kugawa mipira lakini kurudi kwa Wilshere
na usajili wa Cazorla umefanya Arteta asionekane akiwa kiwanjani. Kocha wa
Arsenal Arsene Wenger amekuwa kwenye mazungumzo mara kadhaa na kocha wa England
Hodgson ili kumshawishi asiwatumie sana Walcott na Wilshere kwenye michezo ya
kirafiki ili kuwapa muda wa kupumzika na kupunguza riski ya kuumia kwani
kukosekana kwao uwanjani ni pigo kubwa kwa Arsenal. Katikati ya msimu huu
kulizuka tetesi kuwa Walcott anaweza kuhama Arsenal, lakini uongozi wa Arsenal
kwa kutambua umuhimu wake waliweza kumbakiza kundini. Ki-ukweli hawa wachezaji
ni wakali, Arsene Wenger akikubali kubadilisha sera zake za kuuza wachezaji
wakubwa basi Arsenal itakuwa inatisha sana misimu ijayo.
No comments:
Post a Comment