Thursday, June 20, 2013

Wachezaji wenye maski kuongezeka Chelsea

PREVIEW Luiz Mask
Jana usiku beki wa Brazil na Chelsea David Luiz alivunjika mfupa wa pua baada ya kugongana na mchezaji wa Mexico wakati akijaribu kuokoa mpira langoni mwa Brazil. Kufuatia majereha haya Luiz alitokwa na damu nyingi kiasi cha kumfanya atolewe nje kwa dakika tano ili kupata matibabu na baadaye aliingia tena uwanjani akiwa na pamba puani. Daktari wa timu amesema majeraha haya yatamfanya Luiz atumie Maski ili kuweza kuendelea kucheza kwenye michuano ya Confederation, hivyo, Luiz atakuwa ni mchezaji wa wanne kwa klabu ya Chelsea kutumia Maski akiungana na Torres, Ba pamoja na Peter Cech
On a stretcher: Luiz was led away as they medical team tried to stem the flow of blood
Luiz akitolewa nje baada ya kuumia kwenye mechi ya jana kati ya Brazil na Mexico

No comments:

Post a Comment