Jose Mourinho anatarajiwa kurudi Stamford Bridge hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo urafiki mzuri aliokuwa nao na Bosi wa Chelsea Abramovich. Vile Vile wiki iliyopita Mourinho alisikika akisema anahamu ya kushinda UEFA na timu ya England,
akiulizwa timu gani atayoweza kuhamia alisema ni siri yake, ila alikiri kuwa
akitoka Madrid atahamia England, Mourinho alisema“ Siwezi kuficha kitu, ni
kweli baada ya Spain nakwenda England, hilo lipo wazi, nimekuwa nikiliongelea
hili mara nyingi na nitaendelea kuliongelea, siwezi kuficha kitu. Mourinho
amekuwa akihusishwa sana na Man utd, lakini uwepo wa Sir Alex inasemekana
unamzuia Mourinho. DailyMail, limeripoti kuwa hivi karibuni bosi wa Chelsea Abramo
amekuwa karibu zaidi na Mourinho ikizingatiwa kuwa Rafa Benitez muda wake wa
kuifundisha Chelsea unakaribia kuisha. Abramo anapenda kocha mwenye uhakika wa kuijenga
timu na kuipa timu ushindi ikiwa Mourinho ndiyo chaguo lake la kwanza.
No comments:
Post a Comment