Wednesday, March 27, 2013

Djokovic apigwa na Haas - Miami Open


Mchezaji tenesi namba moja duniani Novak Djokovic amepigwa na Mjerumani Tommy Haas kwa seti mbili mfululizo 6-2, 6-4 katika michuano ya Sony Miami Open. Kipigo hicho kwa Djokovic nichakushitukiza tofauti na matarajio ya wengi ambao walibashiri kuwa Djokovic atatetea tena kombe lake. Andy Murray ndiye mchezaji mkubwa aliyebaki baada ya kumpiga Seppi kwa seti 6-2, 6-4. Murray na Haas wameingia kwenye robo fainali. Murray atakutana na Cilic wakati Haas atacheza na Simon. 

No comments:

Post a Comment