Wednesday, March 27, 2013

Ferguson, sikujua kama ligi ingekuwa nyepesi

Ferguson amesema hakujua kama ligi ingekuwa nyepesi kwa upande wa Man utd msimu huu. Ferguson akiongea na SiriusXM radio alisema “nilijua ligi ingekuwa ngumu sana na yenye ushandi mkali kati ya Man utd na Man city lakini mambo yamekuwa tofauti, tupo mbele kwa pointi 15, siamini kama imekuwa hivi”. Ferguson aliongeza kwa kusema “binafsi nimeshtuka kuona United tupo mbele kawa pointi 15, sio jambo nililotarajia”. Mwaka jana Man City walishinda kombe la ligi kwa kuwazidi United magoli, na ligi ilisubiri hadi mechi ya mwisho kujua mshindi, ila mwaka huu imekuwa tofauti kwani Man utd wamebakiza mechi chache kama watashinda basi watakuwa mabingwa kabla ya ligi kuisha.

No comments:

Post a Comment