|
Messi akiwa hoi baada ya kujisikia kizunguzungu |
Lionel Messi mshambuliaji wa Argentina na Barcelona alijikuta anatapika uwanjani baada ya kujisikia kizunguzungu. Messi alipatwa na tatizo hilo kwenye mechi kati ya Bolivia na Argentina, mechi iliyoisha kwa droo ya goli moja moja. Lionel alishindwa kujizuia uwanjani akajikuta anainama na kutapika kutokana na hali ya hewa nzito nchini Bolivia, nchi ambayo ipo mita 4000 kutoka usawa wa bahari. Wakati Messi anakutwa na hali hiyo mchezaji mwenzake Di Maria alijikuta anatoka nje ya uwanja mara kadhaa na kuvuta oxygen ili aweze kupata nguvu. Wachezaji wengine wa Argentina walishindwa kabisa kucheza baada ya kumwa na vichwa, homa, kupoteza njaa, kizunguzungu na mafua makali. Daktari mmoja nchini Bolivia amesema ni hali ya kawaida kwa wachezaji wasiozoea kucheza kwenye ukanda wa juu kupatwa na matatizo kama hayo. Hata hivyo mechi hiyo ilikwisha vyema kwa droo ya goli moja kwa moja, goli la Argentina likifungwa na Banega wakati goli la Bolivia likifungwa na Moreno.
|
Di Maria akivuta hewa safi (oxygen) |
No comments:
Post a Comment