Monday, March 25, 2013

Mbwana Ally Samata


Mbwana Ally Samata amezaliwa tarehe 13 December 1992 (miaka 21) jijini Dar es Salam, ni mtoto wa askari polisi wa zamani wa jeshi la Tanzania. Mbwana mwenye urefu wa sentimita 179, kilo 79 alianza kuonekana uwezo wake toka akiwa mdogo kabla hajajiunga na African Lyon mwaka 2008 hadi 2010. Kwa kipindi cha miaka miwili African Lyon, Mbwana aliweza kuiongoza vyema safu ya mbele ya timu yake na kuifanya Lyon kuwa timu tishio kwenye ligi ya Tanzania bara. Mwaka 2010 Mbwana alijiunga na Simba ambapo uwezo wake ulimfanya atambulike zaidi ndani na nje ya nchi. Mbwana aliweza kuichezea Simba mwaka mmoja tu kabla ya kuchukuliwa na TP Mazembe ya Kongo kwa shilingi milioni 240.TP Mazembe walimuona Samata katika mechi kati ya Simba na TP Mazembe iliyofanyika Dar es Salaam, mechi ambayo iliisha kwa TP Mazembe kushinda magoli 6-3 kwa ujumla. 


Tokea amefika TP Mazembe, Mbwana ameonekana kuja juu zaidi na kuweza kucheza kwenye kikosi cha kwanza. Club kadha za ulaya zimekuwa zikimzungumzia Samata na kutuma wawakilishi wake kwenda kumchunguza uwezo wake ikiwemo Chelsea.  Kwa mujibu wa TP Mazembe, Samata kwasasa ana dhamani ya dola za kimarekani  laki 7 kutokana na uzoefu aliokuwa nao katika michezo ya kimataifa. Katika mechi ya Taifa Stars na Morocco Samata alifunga magoli mawili na ndiye aliyekuwa akimsha shangwe za mashabiki wa soka wa Tanzania ambao wamekuwa na kiu ya zaidi ya miaka 30 ya kutoiona timu yao ya taifa ikishiriki michuano ya kimataifa tangu mwaka 1980 iliposhiriki kombe la mataifa huru barani Afrika iliyofanyika nchini Nigeria.  

No comments:

Post a Comment