Monday, March 25, 2013

Yanga waanza mazoezi leo

Baada ya kuwa na mapumziko ya siku mbili kikosi cha timu ya Young Africans leo kimeendelea na mazoezi ya asubuhi katika uwanja wa mabatini Kijitonyama ikiwa ni sehem ya maandalizi ya mchezo wake dhidi ya timu ya Polisi Morogoro mchezo utakaofanyika siku ya jumamosi katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Wachezaji walifanya na mazoezi leo ni Said Mohamed, Yusuph Abdul na Ally Mustafa 'Barthez' (magolikipa) Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika, Salum Telela, Oscar Joshua, Godfrey Taita na Juma Abdul (walinzi) Nurdin Bakari, Omega Seme na David Luhende, Reheni Kibingu, (viungo) Jerson Tegete, George Banda, Nizar Khalfani, Didier Kavumbagu na Said Bahanuzi . Wachezaji walokuwa wamejumuika na timu zao za Taifa wataanza mazoezi siku ya jumatano kwa ajili ya safari hiyo ya kuelekea Morogoro. 

No comments:

Post a Comment