Obama amewapongeza Galaxy kwa kushinda kombe la MLS kwa mara ya pili mfululizo,
Obama alitoa pongezi hizo wakati akiwatakia heri wachezaji wa timu ya taifa
katika mechi yao na Mexico. Obama alisema nawapongeza sana Galaxy kwa ushindi,
mtawapa salamu zangu wachezaji wenzenu ambao hawapo hapa, najua wao pia wapo
kwenye timu zao za taifa wakitekeleza majukumu ya kitaifa. Obama pia alipewa
jezi pamoja na mpira wa Galaxy kama shukrani na zawadi kutoka kwa Landon
Donovan akiwakilisha club yake.
No comments:
Post a Comment