Timu ya taifa ya Italy imenusurika kwenye ajali ndege jijini Geneve, Uswisi. Ndege iliyokuwa imebeba wachezaji wa soka wa timu hiyo wakitokea mjini Florence (Italy), ilipigwa na radi kali muda mfupi kabla ya kutua kwenye kiwanja cha ndege Geneva. Wachezaji pamoja na viongozi wa Italy walisika wakishukuru kwa imani zao baada ya ndege hiyo kutua salama. Hakuna mtu yoyote alieumia katika tukio hilo.Timu ya Italy itacheza na Brazil kwenye mechi ya kirafiki inayotarajiwa kuchezwa tarehe 21 mwezi huu Geneva.
No comments:
Post a Comment