Mkongwe, Michael Owen ametangaza kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu. Owen mwenye umri wa miaka 33, ametangaza nia yake leo kwenye official website yake. Owen alianza kujulikana mwaka 1997 alipokuwa Liverpool akiwa na umri wa miaka 17. Akiwa na umri wa miaka 17 aliweza kunyakuwa golden boot kwa kufunga magoli 18. Owen ameshacheza kwenye clubs tano hadi sasa akianzia Liverpool, Real Madrid, Newcastle, Man Utd na sasa yupo Stoke City. Kwenye timu ya taifa amecheza mechi 89 na kufunga magoli 40.
No comments:
Post a Comment