Saturday, July 13, 2013

Tanzania 0 - 1 Uganda

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars leo imeonesha udhaifu baada ya kufungwa goli 1-0 na timu ya Uganda kwenye mechi ya kwanza ya michuano ya CHAN. Uganda ilipata goli kipindi cha kwanza lililodumu hadi mpira unakwisha. Matokeo haya yameondoa kabisa matumaini ya Tanzania kushiriki katika fainali za michuano hii nchini Afrika Kusini kwani ili kusongombele itahitajika kushinda magoli 2-0 kwenye mchezo wa marudiano nchini Uganda wiki mbili zijazo. Wapenzi wa soka walikusanyika kwa wingi uwanja wa taifa wakitegemea kuona soka safi la taifa stars kama walivyocheza dhidi ya Ivory coast, lakini mambo yalikuwa tofauti na wachezaji walionekana wachovu na walipoteza nafasi nyingi. 

No comments:

Post a Comment