Carzola akiwa amepiga makoti pasipo kuamini matokeo licha ya jitihada zake alizozionyesha katika mchezo uliokwisha kwa droo ya bila kufungana kati ya Arsenal na Everton, matokeo haya yanaifanya Arsenal ifikishe pointi 60 ikiwa imecheza michezo 33, wakati wapinzani wake Chelsea wana pointi 58 na wamecheza michezo 31, Tottenham wana pointi 58 na michezo 32, ikiwa Chelsea na Tottenham watashinda michezo yao ya wiki hii wataweza kuipiku Arsenal na kuifanyairudi tena kwenye nafasi ya tano. |
Mchezo wa jana ulizua ugomvi kati ya Wilshere na Mirallas baada ya kulumbana uwanjani lakini ugomvi wao uliendelea hadi mapumziko baada ya Mirallas kumwagia Wilshere maji usoni jambo lililoleta mzozo nje ya uwanja wakati wa mapumziko. FA italiangalia tukio hili na kutoa maamuzi mapema kwani vitendo kama hivi vya utovu wa nidhamu uwanjani vitaweza kuvunja heshima ya soka la Uingereza. . |
No comments:
Post a Comment