Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) linatakiwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na klabu ya Toto African ya Mwanza. Uongozi wa Toto uliiomba TFF kusogeza mbele michezo yake iliyobakia ili waweze kumaliza michezo ya ligi sawa sawa na timu zingine. Toto African ambayo inashikilia nafasi ya nne kutoka mwisho ina pointi 22, imeshacheza michezo 24 na imebakiza michezo miwili iweze kumaliza mechi zake huku kukiwa na timu zingine zimebakiza michezo mitano kitu ambacho kinaweza kupelekea upangaji wa matokeo. Ratiba ya ligi jinsi ilivyosasa inaonesha kuna timu zitamaliza michezo yake siku tofauti na zingine kitu ambacho ni tofauti na uendeshaji wa ligi duniani kote ambapo mechi zote za mwisho wa ligi zinachezwa wakati mmoja na siku moja ili kuepuka kupanga matokeo. Toto African ikiwa inapigania kutoshuka daraja ipo kwenye ushandi mkali dhidi ya JKT Ruvu, Polisi Moro, African Lyon na Mgambo Shooting ambapo timu hizi zinashika nafasi tano za mwisho na zinatofautiana pointi chache kitu ambacho kitazifanya zingojee hadi mechi za mwisho kujua nani atashuka na nani atabaki ligi kuu, ikiwa TFF watasikiliza maombi ya Toto ya kupanga ratiba itakayo zifanya timu zote zimalize mechi za mwisho siku moja.
No comments:
Post a Comment