Saturday, April 20, 2013

Arsenal imerudi nafasi ya tatu

High five: Per Mertesacker (left) celebrates scoring the opening goal with Nacho Monreal
Mertesacker akipongezwa na Monreal baada ya kufunga goli katika mchezo wa leo dhidi ya Fulham, mchezo uliokwisha kwa Arsenal kushinda kwa goli moja kwa bila. 
Klabu ya Arsenal imerudi kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Fulham. Arsenal imefikisha pointi 63 ikiwa imecheza michezo 34 kati ya 38. Arsenal imebakiza michezo minne, kati ya hiyo michezo miwili ni ya nyumbani dhidi ya Man utd na Wigan, na michezo ya ugenini ni dhidi ya QPR na Newcastle. Arsenal ipo kwenye ushindani mkali dhidi ya Chelsea na Tottenham kugombania nafasi ya tatu na nne, nafasi ambazo ni tiketi ya ushiriki kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya (UEFA champions). Kwa mtazamo wa kawaida Arsenal ipo kwenye nafasi nzuri kumaliza ndani ya "top four" zaidi ya Chelsea na Tottenham kwa kuzingatia ugumu wa michezo iliyobakia kwa timu zote. Chelsea imebakiza mechi ngumu tatu dhidi ya Liverpool, Tottenhm na Man utd wakati Tottenham imebakiza mechi ngumu mbili dhidi ya Man city na Chelsea. Arsenal mechi ngumu iliyobakia ni moja dhidi ya Man utd, mechi ambayo Arsenal watacheza nyumbani kwenye uwanja wa Emirates tofauti na Chelsea ambayo itakuwa ugenini katika mechi zake dhidi ya Liverpool na Man utd. Arsenal wanangojea kwa hamu matokeo ya mechi zitakazochezwa jumapili April 21 ambazo zitakutanisha Man City vs Tottenham na Liverpool vs Chelsea. Matokeo ya mechi hizi yatatoa majibu kwa kiasi kikubwa ya ushindani uliopo kati ya timu hizi tatu katika kugombea nafasi ya tatu na ya nne.       

Video ya goli alilofunga Mertesacker katika mechi ya leo kati ya Arsenal dhidi ya Fulham

No comments:

Post a Comment