Sunday, April 21, 2013

Uhamisho wa Bale kuweka rekodi ya dunia

Klabu ya Tottenham inataka kuweka rekodi ya dunia ya uhamisho wa mchezaji wake tegemezi Gareth Bale baada kutanganza bei ya mchezaji huyo ambayo ni paundi milioni 100. Mwenyekiti wa Tottenham Levy alisema klabu yake inachohitaji ni hizo pesa tu ili kumwachia Bale kuondoka Tottenham, kauli ambayo wengi wameitafsiri kama tishio ili vilabu vinavyomuhitaji vikate tamaa. Hadi sasa uhamisho wa Cristiano Ronaldo wa paundi milioni 80 kutoka Man utd kwenda Real Madrid ndiyo unashikilia rekodi ya dunia, lakini, kama Tottenham watafanikiwa kuumuza Bale kwa paundi milioni 100 uhamisho huo utazidi ule wa Cristiano Ronaldo na Bale ndiye atashikilia rekodi ya dunia. Klabu ambazo zimeshatangaza kumhitaji Bale ni pamoja na PSG, Real Madrid na Bayern Munich. Klabu hizi tatu zinazomuhitaji Bale zinauwezo wa kulipa paundi mil 100, ila kubaki au kuondoka kwa Bale kutategemea matokeo ya mwisho ya ligi kuu nchini Uingereza, kwani uongozi wa Tottenham umesema hautakuwa tayari kumuuza Bale kama Tottenham itapata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya (UEFA champions) msimu ujao.     

No comments:

Post a Comment