Monday, August 19, 2013

Alex Oxlade-Chamberlain nje wiki sita

Agony: Oxlade-Chamberlain was clearly in a lot of pain as he lay on the turf at the Emirates
Mshambuliaji wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain, atalazimika kukaa nje ya benchi kwa wiki sita baada ya kuumia vibaya kwenye goti lake la kushoto. Alex alipata majeraha kwenye mechi kati ya Arsenal na Aston Villa baada ya kugongana na beki wa Aston Villa, Antonio Luna. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amethibitisha kutokuwepo kwa Alex ndani ya dimba kwa wiki sita baada ya vipimo kuonesha kuwa ameumia vibaya na atahitaji matibabu makubwa. Arsenal inakabiliwa na mechi ngumu ya kuwania kufuzu kwenye michuano ya Uefa dhidi ya Fenerbache siku ya jumatano. Kukosekana kwa Alex kwenye mechi hii itakuwa ni pigo kwa klabu ya Arsenal ambayo ni dhaifu kwenye safu ya ushambuliaji.  
Ouch: Alex Oxlade-Chamberlain was carried off after a collision during Arsenal's match against Aston Villa

No comments:

Post a Comment