Timu ya Taifa ya Ivory Coast vijana chini ya umri wa miaka 17 leo wametwaa ubingwa wa Afrika chini ya miaka 17 baada ya kuwafunga Nigeria kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya dakika 120 kumalizika kwa goli 1-1. Ushindi huu kwa Ivory Coast ni wa kwanza tokea waanze kushiriki katika michuano hii. Michuano hii iliyofanyika nchini Morocco imeshudia pia Tunisia wakiibuka washindi wa tatu baada ya dakika 120 kuisha goli 1-1 na Tunisia kuwafunga wenyeji Morocco kwa mikwaju ya penati 11 -10 |
No comments:
Post a Comment