Wikiendi hii kulifanyika mechi kati ya Rafiki wa Ronaldo vs Rafiki wa Bebeto ikiwa ni mechi maalumu ya ufunguzi wa uwanja wa Maracana wenye uwezo wa kubeba watazamaji 78,838, uwanja huu utatumika kwenye mechi ya fainali ya kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014. Uwanja wa Maracana ulikuwa umefungwa kupisha matengezo kwa takribani miaka miwili na nusu umefunguliwa huku Rafiki wa Bebeto wakiambulia kipigo cha goli 8-5 dhidi ya Rafiki wa Ronaldo, katika mchezo huo wa kirafiki Ronaldo alifanikiwa kufunga goli zuri dakika ya 32 likiwa ni goli la saba kwa upande wa timu yake wakati goli la mwisho kwa upande wa Marafiki wa Bebeto lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Bebeto mwenyewe. Angalia highlights za mechi hiyo kwenye video ya chini
Mkongwe Bebeto akimtoka beki katika mechi kati ya Marafiki wa Ronaldo na Marafiki wa Bebeto, mechi iliyomalizika kwa Marafiki wa Ronaldo kuibuka na ushindi wa goli 8-5 dhidi ya marafiki wa Bebeto
Taswira ya uwanja wa Maracana unavyoonekana baada ya matengenezo ya miaka miwili na nusu, uwanja huu ndiyo utatumika kwenye mechi ya fainali ya kombe la dunia nchini Brazili mwaka 2014
Mkongwe Ronaldo akiachia shuti kufunga goli la saba kwa timu yake
No comments:
Post a Comment