Mwenyekiti wa Kamati ya Uendelezaji wa jengo dogo la Yanga SC, liliopo Mtaa wa Mafia, Kariakoo, Dar es Salaam, Ridhiwani Jakaya Kikwete ameteua Wajumbe kadhaa wa kumsaidia kazi hiyo, wakiwemo wanasheria wawili na wataalamu wa Taasisi za Fedha. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Ridhiwani alisema katika uteuzi wa Kamati hiyo, amezingatia utaalamu, uzoefu na mahusiano mazuri na watu. Aliwataja Wajumbe wa Kamati ya Wataalamu kuwa ni Makamu wake, Issa Hajji Ussi na Wajumbe Isaac Chanji, Mbaraka Igangula, Jaji John Mkwawa, mtumishi ya Beki ya Uwekezaji Tanzania (T.I.B.), Alan Magoma, Mwanasheria mkongwe, Mavale Msemo na mtumishi mwingine wa Benki, Charles Palapala. Ridhiwani alisema watu wengi wanatoka taasisi za fedha, kwa sababu zoezi hili linahitaji fedha, mambo ya ubia na uwekezaji.
No comments:
Post a Comment