Monday, April 8, 2013

Ligi kuu daraja la pili kanda ya kati yaendelea

Ligi kuu daraja la pili kanda ya kati imendelea tena leo baada ya Polisi Dodoma na Chamwino ikulu kwa Rais kutoka droo ya 0-0 katika mchezo ulifanyika katika uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma. Mtanange huo uliopigwa jioni ya leo (8/4/13) ulikuwa mkali ambapo timu ya Polisi ilishindwa kabisa kuhimili mikikimiki ya vijana wa ikulu wakiruhusu mashambulizi langoni mwao kwa takribani dakika zote za mchezo lakini Chamwino alishindwa kuzitumi vyema nafasi zao na kupelekea hadi mwisho wa mchezo Polisi 0 - 0 Chamwino. Katika mechi nyingine iliyochezwa jana jioni (7/4/13) timu ya CDA watoto wa nyumbani chini ya kocha wake Juma Masugu aliyewahi kuichezea timu hiyo miaka ya 90 ilitoka sare ya magoli 2-2 na timu ya The Gunners( wanajeshi kutoka Ihumwa). Katika mchezo huo kipindi cha kwanza kilikwisha kwa CDA kuwa nyuma kwa magoli mawili lakini iliweza kuyarudisha magoli yote katika kipindi cha pili baada ya kuongeza nguvu. Ligi daraja la pili kanda ya kati inashirikisha timu kutoka Singida, Tabora, Mpwapwa, Kondoa na Dodoma mjini. Bingwa wa kanda atawakilisha katika ligi daraja pili Tanzania. 
Wachezaji wa Polisi (bluu) wakisalimiana na Chamwino (Njano) kabla ya mchezo

No comments:

Post a Comment