Monday, April 8, 2013

Man City yaichapa United, Mancini atimiza ahadi yake

Timu ya Man City imeweza kuwapa furaha mashabiki wake ikiwa ni ahadi waliojiwekea wachezaji kama shukrani baada ya kulikosa kombe la ligi ambalo Man utd ndiyo wenye nafasi kubwa ya kulichukua. Man City jana usiku iliweza kuilipiza kisasi kwa Man utd baada ya kuichapa goli 2-1 katika uwanja wa nyumbani wa Man utd. Magoli ya Man city yalifungwa na Milner (51') na Aguero (79') wakati goli la kufutia machozi la Man utd lilifungwa na Kompany dk ya 59' likiwa ni goli la kujifunga. Kabla ya mchezo wa leo kocha wa Man city alisema wanakwenda kuwaonesha Man utd kuwa wao hakustahili kuzidiwa pointi 15, kauli ambayo ameweza kuitimiza. 

Mchezo ulianza kwa kasi tokea mwanzo hadi mwisho ukiwa ni wa mashambulizi ya pande zote lakini Man utd walionesha kuzidiwa hadi kupelekea Man city kujipatia magoli mawili. Udhaifu wa safu ya ulinzi ya Man utd umejionesha wazi ambapo Jones alishindwa kabisa kuliziba pengo la Vidic, vilevile washambuliaji wa Man utd akiwemo Rooney na Van Persie hawakuweza kuonesha mchezo mzuri ambao ulitarajiwa na mshabiki wa Man utd kwani walishindwa kabisa kupita kwenye ngome ya Man city. Matokeo ya mechezo huu umeifanya Man utd iendelee kungojea hadi mechi za mwisho ili kujihahakikisha ubingwa baada ya Man city kupunguza gepu kutoka tofauti ya pointi 15 hadi pointi 12. 

No comments:

Post a Comment