Monday, April 29, 2013

Nadal na Maria washinda Barcelona na Stuttgart

Rafael Nadal (Kushoto) akiwa ameshikilia kombe aliloshinda katika michuano ya Barcelona open baada ya kumshinda mpinzani wake Nicolas (kulia) kwa seti mbili mfululizo 6-4, 6-3. Hii inakuwa ni mara ya nane kwa Rafael Nadal kushinda Barcelona open ikiwa ni michuano ya nyumbani akiwa kama raia wa Hispania. Nadal aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu ameanza kurudi kwenye kiwango chake licha ya kufungwa na Djokovic katika michuano iliyopita ya Monte Carlo. Nadal ameahidi kufanya vizuri zaidi kwenye michuano inayofuata ya French open ambayo yeye hujigamba kuwa ndiyo michuano yake akiwa anashikilia rekodi ya kushinda mara saba zaidi ya wenzake. 
Maria Sharapova akiwa amekaa juu ya gari aina ya Porsche huku ameshikilia kikombe baada ya kushinda katika michuano ya Stuttgart. Maria ameweza kutetea kikombe hiki baada ya kumfunga Li Na kwa seti mbili mfululizo 6-4,6-3 na kunyakua gari pamoja na kikombe. Maria amesema ushindi huu ni chachu ya ushindi kwenye michuano migumu inayofuata ya French open ambayo wachezaji wote nguli wa tenesi watashiriki. Maria Sharapova kwasasa anashikilia nafasi ya pili duniani kwenye tenesi akiwa na pointi 10240 wakati Serena Williams anashikilia nafasi ya kwanza kwa pointi 11115. 

No comments:

Post a Comment