Sunday, March 24, 2013

Mtoto wa Pele, Joshua anakuja juu

Mwanasoka bora wa zamani Pele, ambaye hadi sasa hakuna mtu aliyeweza kuvunja rekodi zake duniani amerudi tena dimbani lakini kupitia mtoto wake Joshua mwenye umri wa miaka 16. Akiandika kwenye Twitter yake Pele alisema “Nina furaha kumuona mtoto wangu Joshua akiwa kwenye jezi za Santos”  Pele alianza kucheza soka Santos akiwa na miaka 15 na kuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mdogo kushinda kombe la dunia. Pele alifunga magoli 1000 akiwa Santos na hadi leo timu ya Santos inasherekea “Pele Day” kila mwaka kumkumbuka. Pele anaamini kijana wake Joshua ndiyo ameanza kuelekea alipopita yeye na ipo siku atakuwa na jina kubwa duniani kama yeye au zaidi yake.   

No comments:

Post a Comment