|
Cesc na Daniella walipokuwa kwenye harusi ya Iniesta jijini Barcelona |
Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas yupo kwenye harakati za
kuimarisha mapenzi yake na Daniella Semaan baada ya kuonesha nia yake ya
kununua nyumba aliyokuwa anaishi Daniella na mpenzi wake wa zamani bwana Taktouk. Mwaka 2011 Fabregas aliyaingilia mapenzi kati ya Daniella na Taktouk kitu ambacho
kilimkera bwana Taktouk. Daniella mwenye umri wa miaka 38 aliweza kumnasa
Fabregas katika hotel moja jijini Barcelona wakati Cesc alipokuwa ameketi na
rafiki zake, Daniella alijipitisha na kudondosha kikaratasi juu ya
meza aliyokaa Fabregas, kikaratasi hicho kilikuwa kimeandikwa jina, namba ya
simu na mahali anapoishi Daniella, bila ya kuchelewa Cesc alipopata namba na
jina lake alimpigia simu na kuomba wakutane na baadaye kuelekea Dubai kwa
mapumziko. Baada ya Taktouk kugundua mpenzi wake anatoka na Cesc akaamua kupiga
mnada nyumba waliokuwa wanaishi kitu ambacho kilimkera Daniela na kuamua
kutafuta dalali ili ainunue hiyo nyumba yeye na Cesc, lakini bwana Taktouk
aligundua hilo dili la chini chini na kugoma kuuza nyumba hiyo iliyopo London. Hali hii imemfanya
Cesc achanganyikiwe kwa maana mpenzi wake Daniella anaitaka hiyo nyumba wakati
bwana Taktouk amegoma kuwauzia. Hadi sasa bwana Taktouk ameendelea na msimamo wake wa kutouza nyumba kwa Daniella kitu ambacho kinakatisha usingizi wa wawili hao. Daniella ana umri wa miaka 38, wakati Cesc
miaka 25 toufauti ya miaka 13, walifanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza mwaka
huu akiwa ni mtoto wa tatu kwa Daniella, watoto wengine wawili Daniella alizaa
na bwana Taktouk.
|
Cesc na Daniella walipokuwa Dubai kwenye mapumziko ya siku za mwazo ya mapenzi yao |
No comments:
Post a Comment