Tuesday, April 9, 2013

Ramires, Oscar na Luiz wamkaribisha Ester

Wabrazili wa Chelsea Ramires, Oscar na Luiz wamemkaribisha Mbrazili mwenzao Ester mchezaji wakike aliyesajiliwa na Chelsea akitokea WFC ya Russia. Ramires na wenzake waliungana na Ester ili kumpa kampani Mbrazili mwenzao kwenye siku yake ya kwanza darajani. Ester ni mchezaji wakike wa kwanza Mbrazili kusajiliwa na Chelsea katika FA Women’s Super League.Ester ameshacheza mechi 56 katika timu ya taifa na ameshashiriki mara tatu katika michuano ya olimpiki na timu ya taifa. Ester kiungo mkabaji akihojiwa na Chelsea TV alisema “nina furaha sana kuwa hapa (Chelsea), ni timu kubwa na ninajisikia nipo nyumbani zaidi kuwepo pamoja na Ramires, Oscar na Luiz. Ester kabla ya kujiunga na Chelsea alishacheza katika vilabu vya Santos, WFC Russia na Juventus

Luiz,Ester, Ramires na Oscar

No comments:

Post a Comment