Kiungo wa Chelsea Frank Lampard amesema wachezaji wengi wa
Chelsea akiwemo yeye hawana uhakika wa namba. Lampard akinukuliwa na The Daily
Telegraph amesema “sidhani kama kuna mchezaji wa Chelsea ukiondoa golikipa na
mabeki wenye uhakika wa kucheza mechi yoyote. Mimi nimekuwa kwenye kiwango cha
juu sana hivi sasa lakini sina uhakika kama nitacheza dhidi ya Man City, jambo
hili linategemea na mapenzi ya kocha na mahusiano kati ya mchezaji na kocha”. Lampard
alimalizia kwa kusema “Napenda sana kucheza mechi zote za Chelsea lakini kocha
ndiye mwenye maamuzi ya mwisho kuchagua nani wa kucheza”. Wachambuzi wa maswala
la soka wamesema kauli hii ya Lampard imeonesha wazi kuwa kiungo huyu hana
mahusiano mazuri na kocha wake Benitez jambo ambalo linakoleza zile tetesi kuwa Lampard atahamia Galaxy ya Marekani
msimu ujao. Chelsea inashuka dimbani jumapili kukutana na Man City katika
mchezo wa nusu fainali ya FA, mchezo utakao fanyika kwenye uwanja wa Wembley.
No comments:
Post a Comment