Wednesday, April 10, 2013

Ubaguzi wa rangi, UEFA imetoa mapendekezo makali

Shirikisho la mpira wa miguu barani ulaya UEFA kupitia katibu mkuu wake Gianni Infantino imetoa mapendekezo yanayoweza kutumika kutoa adhabu kali kwa mashabiki, wachezaji na timu zitakazohusika na aina yoyote ya ubaguzi wa rangi. Katibu huyo alisema UEFA  imependekeza kuwa, mashabiki watakao husika na ubaguzi basi kiwanja husika kitafungiwa kwa muda, kama mchezaji au afisa wa club atahusika atafungiwa kucheza/kushiriki kwenye mechi kumi, na kama mchezaji au washabiki watarudia tena kiwanja husika au mchezaji atafungiwa kwa muda mrefu na kulipa faini ya paundi 42,700, UEFA inatarajia kuyawakilisha mapendekezo haya kwenye mkutano mkuu utakaofanyika mwezi May jijini London. 
Boateng akihutubia kuhusu ubaguzi kwenye mkutano wa haki za binadamu Umoja wa mataifa (UN)
UEFA imetoa mapendekezo haya baada ya vitendo vya ubaguzi kushamiri. Mwaka jana John Terry na Luis Suarez walipewa adhabu baada ya kuthibitishwa kufanya ubaguzi ambapo Terry alisimamishwa kucheza mechi nne na faini ya paundi 220,000 wakati Suarez alifungiwa mechi nane na faini ya paundi 40,000, pamoja na adhabu hizo UEFA na FIFA imekuwa ikihamasisha kukomesha ubaguzi wa rangi kwa wadau wake wote kupitia njia mbalimbali ikiwemo matangazo kwenye viwanja lakini bado baadhi ya mashabiki wameendelea  kufanya vitendo vya kibaguzi hususani kwa wachezaji wenye asili ya Kiafrika, Asia na Amerika Kusini. 
Suarez alipokuwa anamtukana Evra siku Man utd ilipokuwa inacheza na Liverpool, kitendo ambacho kilimfanya apewe adhabu ya kutocheza mechi nane. 
Kitendo cha Kevin Prince Boateng kiungo wa Ac Milan kutoka nje ya uwanja baada ya kufanyiwa kitendo cha ubaguzi ndicho kimewezesha UEFA na FIFA kutafakari njia kali zaidi za kupambana na ubaguzi ikiwemo hizi zilizopendekezwa leo na UEFA. Boateng alioneshewa ndizi na mashabiki wa Pro Patria kwenye mechi kati ya AC Milana na Pro Patria ikiwa ni ishara kuwa Boateng amefanana na nyani, baada ya kitendo hicho Boateng alikasirika na kutoka nje ya uwanja, baada ya kitendo hicho, Boateng katika hotuba yake UN alisema ubaguzi ni kirusi kilicho ndani ya watu ambacho hakina faida yoyote. 
Boateng akitoka nje ya uwanja siku alipooneshewa ndizi na mashabiki wa Patria
UEFA na FIFA hadi sasa wanafikiria njia za kupambana na vitendo hivi na wametoa ruhusa kwa wadau mbalimbali kutoa maoni yao ila kupata sheria muafaka zitakazo weza kupambana na kukomesha ubaguzi wa rangi. Wadau wanaweza kutuma maoni yao kupitia email address ya FIFA na UEFA au tembelea tovuti husika. 
Siku Boateng alipokutana na Raisi wa FIFA Blatter kuwasilisha mapendekezo yake ya kukomesha ubaguzi wa rangi

No comments:

Post a Comment