Thursday, April 18, 2013

Unakubaliana na mawazo ya David James?????

David James
David James golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya England amesema makocha wenye asili ya Kiafrika hawapati nafasi ya kufundisha klabu kubwa kwenye ligi ya England kwasababu hawana uwezo wa kutosha. Akiongea na gazeti la Sport 360 James alisema “makocha weusi hawana uwezo, hakuna haja ya kuwapa kazi ya ukocha, wamiliki wengi wa timu za mpira wapo tayari kusajili wachezaji weusi ila sio makocha weusi kwasababu hawana vigezo vya kufundisha timu kubwa". 

Chri Hughton
James aliendelea kusema, "kati ya klabu 92 za England kuna makocha weusi watano tu na kati ya hao ni kocha mmoja tu aliyefanikiwa ambaye ni kocha wa Norwich Chri Hughton. Hughton amefanikiwa kwasababu ana utaratibu mzuri wa yale anayoyapanga na kuyafanya, lakini wengine wote waliobakia hawawezi kufika popote na sio kweli kwamba jambo hili linahusisha ubaguzi wa rangi kama vile wengi wanavyofikiria” hayo ni maneno ya James ambaye alishawahi kuwa mchezaji wa Liverpool, Man City na Aston Villa kwasasa yupo nchini Iceland kwenye klabu ya IBV. 

No comments:

Post a Comment