Thursday, April 18, 2013

Rooney kafeli kucheza kama kiungo

Night to forget: Wayne Rooney was hooked off by Sir Alex Ferguson after 71 minutes at West Ham following an ineffective performance in midfield
Hivi Sir Alex Ferguson anataka kumaliza kipaji cha Rooney??? Imepita mwaka sasa tokea Rooney abadilishwe nafasi kutoka ushambuliaji hadi kuwa kiungo. Tokea Rooney aanze kucheza nafasi ya kiungo amekuwa akichemsha sana lakini Sir Alex hajataka kulifanyia kazi zaidi ya kuendelea kumpanga kama kiungo. Picha hii inamuonesha Rooney akitoka dakika ya 71 katika mechi kati ya West Ham na Man utd ambapo Rooney alikuwa akicheza nafasi ya kiungo, lakini alishindwa kabisa kuimudu jambo lililofanya atolewe na kuingia Giggs.
Little consolation: Rooney is greeted by Ferguson as he is replaced by Ryan Giggs with United trailing 2-1
Sir Alex akimfariji Rooney baada ya kutoka nje ya uwanja, lakini Rooney alionekana kuchuna kwasababu hajaridhika na nafasi anayocheza. Ujio wa Van Persie na Kagawa pamoja na kiwango kizuri cha Danny Welbeck ndiyo kimemfanya Sir Alex kumsahau Rooney kwenye nafasi ya ushambuliaji.
Picha hii inaonesha takwimu za uchezaji wa Rooney katika mechi ya West Ham akiwa kama kiungo. Takwimu zinaonesha kati ya dakika 71 alizocheza Rooney aliweza kugusa mpira mara moja tu kwenye kumi na nane za lango la West Ham. Pia katika mechi hii Rooney aliweza kupiga pasi 65 tu wakati Carrick ambaye ni kiungo mkabaji alipiga pasi 117, vile vile Rooney aliweza kupiga pasi ya mwisho moja tu ambayo hakuzaa matunda dhidi ya pasi tano za Carrick. Tathimini zinaonesha na kuthibisha wazi kabisa kuwa Rooney amefeli kucheza kama kiungo ila Sir Alex hajataka kukubali kuwa naye anaweza kukosea.  

No comments:

Post a Comment