Tuesday, May 14, 2013

Arsenal, safari ya UEFA champions imewadia

Pure ecstasy: Theo Walcott celebrates after scoring for the Gunners (below) with 63 minutes gone
Four-some: Walcott and Aaron Ramsey lead the celebrations after the Welshman's strike at the Emirates
Wachezaji wa Arsenal wakicheza kushangilia goli la nne lililofungwa na Ramsey dakika ya 71 na kuifanya timu hiyo kuibuka na ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Wigan. Kwa matokeo haya Arsenal wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kushiriki michuano ya UEFA champions msimu ujao kwani wamefikisha pointi 70 ambazo ni pointi moja mbele ya Tottenham. Timu zote zimebakiza mchezo mmoja na Arsenal inahitaji pointi mbili tu ili kujihakikishia nafasi ya nne. 

Wigan yaweka historia England 

Time's up: Wigan will play their football in the npower Championship from next season
Klabu ya Wigan jana iliweka historia katika soka nchini England kwani haijawahi kutokea timu kushinda FA cup na msimu huo huo ishuke daraja, hii itakuwa ni historia ya kwanza ambayo Wigan wameianzisha. Jumamosi iliyopita Wigan waliifunga Man city goli 1-0 na kuwa mabingwa wa FA cup mwaka huu lakini kipigo cha jana dhidi ya Arsenal kimeifanya klabu hiyo kusahau furaha za ushindi wa jumamosi

No comments:

Post a Comment