Wednesday, May 15, 2013

Chelsea na Arsenal zinatarajiwa kukutana

Shirikisho la mpira nchini Uingereza limeshajipanga kuandaa mechi kati ya Arsenal na Chelsea ili kupata mshindi wa tatu wa ligi kama pointi za mwisho za timu hizo zitakuwa zimelingana. Chelsea kwasasa wana pointi 72 na tofauti ya magoli 35 wakati Arsenal wana pointi 70 na tofauti ya magoli 34. Kama chelsea atatoka droo kwenye mechi ya mwisho dhidi ya Everton atakuwa na pointi 73 na toufati ya magoli 35 na wakati huo huo kama Arsenal atashinda kwa tofauti ya goli moja dhidi ya Newcastle basi Arsenal pia watafikisha pointi 73 na tofauti ya magoli 35 ambayo ni sawa sawa na Chelsea jambo ambalo litazifanya timu hizo zicheze mechi ya kuamua mshindi wa tatu ambaye atapita moja kwa moja kushiriki michuano ya kombe la klabu bingwa ulaya na mshindi wanne itabidi ashiriki kwenye play off ili kupata nafasi ya kushiriki klabu bingwa hatua ya makundi. Zifutatazo ni chati zinazoonesha msimamo wa Chelsea na Arsenal kwasasa na baada ya matokeo ya mwisho kama Chelsea atatoka droo na Arsena kushinda kwa tofauti ya goli moja 

Msimamo ulivyosasa 
TEAM
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
CHELSEA
37
21
9
7
73
38
35
72
ARSENAL
37
20
10
7
71
37
34
70

Msimamo unavyotarajiwa kuwa baada ya mechi za mwisho 
TEAM
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
CHELSEA
38
21
10
7
73
38
35
73
ARSENAL
38
21
10
7
73
38
35
73

No comments:

Post a Comment