Baada ya kudumu kwa miaka 20 na udhamini wa Nike, klabu ya
Arsenal imeamua kusaini mkataba mpya na kampuni ya Puma mkataba utakao gharimu
kiasi cha paundi mil 170 ambapo kila mwaka Arsenal watakuwa wakipata udhamini
wa paundi mil 30 kwa kipindi cha miaka mitano. Ivan Gazidis ambaye ni mkurugenzi
mtendaji wa Arsenal amethibitisha hilo na amesema klabu ya Arsenal itaanza
kuvaa jezi za Puma baada ya msimu ujao kuisha. Nike walioanza kuidhamini
Arsenal toka mwaka 1993 mkataba wao utakwisha mwishoni mwa msimu ujao na
maongezi ya awali kati ya Arsenal na Nike hayakuweza kufikia muafaka ndiyo
maana Arsenal wakaamua kuachana na Nike kwenda Puma. Hivyo Arsenal itakuwa ni
timu kubwa ya kwanza barani Ulaya kudhaminiwa na Puma kwani klabu kubwa zote za
Italy, England, Hispania, Ufaransa na Ujerumani zina udhamini wa Adidas na
Nike. Kwenye ligi ya England klabu zenye udhamini wa Puma ni Newcastle
na Reading.
No comments:
Post a Comment