Kiungo wa Barcelona Adres Iniesta amesema kipigo cha Bayern
Munich cha goli 7-0 walichokipata kwenye nusu fainali ya klabu bingwa barani
Ulaya bado kinamuuma. Adres alisema ‘ kipigo cha Bayern kilikuwa kibaya sana,
tokea siku ile hadi leo bado naumia sana, angalau leo najisikia vizuri kidogo, lakini ule usiku wa mechi sikulala vizuri na nilipoamka niliona siku inakwenda
vibaya tofauti na nivyozoea. Ilikuwa haiwezekani kusahau kwa mara moja, itachukua
muda mrefu kwangu na wenzangu pia, ila huu ni muda wa kujipanga kwa msimu ujao
lazima tutapigana kurudisha heshima yetu”. Iniesta aliyasema hayo alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari wiki hii akielezea mipango ya Barca kwa msimu
ujao kwenye klabu bingwa ulaya. Mbali ya kutolewa kwenye UEFA champions, Barcelona
imeanza kujiandaa kusheherekea ubingwa wa ligi ambao wanatarijia kuunyakuwa kwenye
mchezo wao unaofuata dhidi ya At. Madrid utakaochezwa jumapili ya tarehe 12/5/13.
No comments:
Post a Comment