Friday, May 17, 2013

Messi ni moja ya sababu ya mimi kustaafu - Beckham

Mkongwe David Beckham jana alitangaza rasmi kustaafu soka baada ya kucheza kwa takribani miaka 20. Alipokuwa akihojiwa sababu zilizomfanya kustaafu, Beckham alitaja sababu nyingi ikiwemo kuwaachia vijana wenye umri chini yake kuonesha uwezo wao lakini pia alimtaja Messi kuwa ni sababu moja wapo. Beckham alisema hayo alipokuwa akihojiwa na mtangazaji wa TV ambaye alikuwa pia ni mchezaji mwenzake Gary Neville, Beckham alisema huku akicheka” nahisi moja ya sababu zilizonifanya nijione muda wangu umepita, ni pale ambapo Messi alikuwa akikimbia akanipiga chenga na kunipita bila ya kujua cha kumfanya katika mechi ya nyumbani kati ya PSG na Barcelona April 2”. Beckham pia alisema licha yakuwa amepitwa na wakati kiasi cha kushindwa kupambana na damu changa lakini ameweza kujitahidi kucheza nao bila kuonesha utofauti mkubwa. David Beckham anatarajiwa kucheza mechi yake ya mwisho siku ya tarehe 18 kati ya PSG na Brest.  

No comments:

Post a Comment