Friday, May 17, 2013

Mata, Lampard, Oscar wapata tuzo za ndani

Double delight: Juan Mata was named Chelsea Player of the Year and Players' Player of the Year
Juan Mata akionesha vikombe vyake alivyozawadiwa kama mchezaji bora wa Chelsea wa mwaka huu. Zawadi hii imekuja kwa Mata akiwa ndiye mchezaji  aliyesaidia timu kwa kiasi kikubwa, kwani msimu huu ameshafunga magoli 19 na amewezesha magoli 28 kufungwa. Tuzo hii inakuwa ni ya pili mfululizo kwa Mata kwani mwaka jana pia aliweza kushinda. 
Golden boys: Frank Lampard receives special recognition award from Bobby Tambling
Frank Lampard akiwa ameshikilia tuzo yake akiwa kama mchezaji mwenye magoli mengi kuliko wote kwenye historia ya klabu ya Chelsea. Bobby Tambling ndiye mchezaji aliyekuwa na magoli mengi kuliko wote ndani ya klabu ya Chelsea (magoli 202) lakini wiki iliyopita Lampard alifikisha magoli 203 hivyo kumzidi Tambling. 
Next generation: Lampard presents Nathan Ake with Young Player of the year award
Nathan Ake akiwa ameshika tuzo ya mchezaji kijana
Big hand: John Terry congratulates Oscar as he goes to collect goal of the season award
Oscar akisimama kwenda kuchukua tuzo yake ya goli bora la mwaka alilofunga dhidi ya Juventus kwenye michuano ya UEFA. Chini ni video inayoonesha goli hilo. 
Goli la Oscar dhidi ya Juventus

No comments:

Post a Comment