Sunday, May 12, 2013

Scholes kumfuata Sir Alex Ferguson

Kiungo mkongwe wa Manchester United Paul Scholes ametangaza rasmi kustaafu soka kwa mara ya pili. Scholes alishatangaza kustaafu soka mwaka 2011 lakini Sir Alex alimuita tena kujiunga na kikosi cha United mwaka 2012 mwezi wa kwanza ili kuimarisha sehemu ya kiungo ya klabu hiyo. Scholes aliweza kucheza mechi kadhaa licha yakuwa kiwango chake hakikuwa kama ilivyotarajiwa kutokana na umri wake. Scholes mwenye miaka 38 amethibitisha kustaafu kwa mara ya pili na kusema hatarudi tena dimbani ili awaachie vijana nafasi, licha yakuwa ataendelea kushughulika na kazi mbalimbali za klabu hiyo akiwa kama balozi wa Man utd. Scholes anatarajiwa kucheza katika mechi ya kumuaga Sir Alex Ferguson dhidi ya Swansea itakayofanyika katika uwanja wa Old Trafford, mechi ambayo itakuwa ya mwisho kwake pia ndani ya dimba la Man utd. Scholes alijiunga na United mwaka 1993 hadi leo ameshacheza mechi 491 na kufunga magoli 107 kwa Man utd na kwenye timu ya taifa ameshacheza mechi 66 na kufunga magoli 14. 

No comments:

Post a Comment