Kocha wa Manchester City Roberto Mancini anatarajiwa
kufukuzwa kazi wiki mbili zinazokuja na kumuachia nafasi hiyo kocha wa Malaga
Manuel Pellegrini. Taarifa hizi zimetoka ndani ya uongozi wa Man city bila
kutajwa majina ya waliotoa taarifa hizi kwasababu muda wa kutangaza rasmi bado haujafika. Likielezea swala
hili, gazeti la Sportmail la Uingereza limesema Mancini aliwekewa malengo
mawili mwaka huu ili aweze kuendelea kuwa kocha wa klabu hiyo. Lengo la kwanza lilikuwa, kutetea ubingwa wa ligi kuu na lengo la pili Mancini alitakiwa kuhakikisha Man city inafikia hatua ya robo fainali za klabu
bingwa barani Ulaya (UEFA champions) malengo ambayo ameshindwa kuyatimiza. Kwa sababu
hizi ndiyo maana uongozi wa Man city umeamua kumfukuza kazi Mancini. Vilevile taarifa hizi zilisema hata
kama Mancini angeweza kushinda FA bado alikuwa anafukuzwa kazi kwasababu kombe
la FA halikuwepo kwenye malengo ya mwaka huu ya klabu ya Man city. Roberto
Mancini (48) alijiunga na Man city mwaka 2009 akitokea Inter Milan hadi sasa ameweza
kushinda makombe matatu akiwa na Man city ambayo ni kombe la ligi (2012), FA
cup (2011) na Community shiled (2012).
|
Roberto Mancini akisalimiana na uongozi wa Man city baada ya mechi ya fainali dhidi ya Wigan kumalizika ndani uwanja wa Wembley (Kulia ni bwana Khaldoon Al Mubarak mmiliki wa Man city) |
|
Mancini akikatisha mbele ya umati wa watu akiwa ameangalia chini kwa aibu baada ya Man city kufungwa na Wigan katika mchezo wa fainali za FA cup. |
|
Pellegrini kocha mkuu wa Malaga anayetarajiwa kuchukua mikoba ya Mancini hivi karibuni |
No comments:
Post a Comment