Wednesday, May 29, 2013

Tetesi za usajili barani ulaya wiki hii 29 May 13


Fabregas na Man utd 
David Moyes kocha mpya wa Man utd anajiandaa kumsajili Cesc Fabregas wa Barcelona baada ya klabu hiyo kuonesha nia ya kumuuza mchezaji huyo ambaye amepata wakati mgumu ndani klabu hiyo kupata namba ya kudumu. Man utd wamejiandaa kutoa dau la paundi mil 25 kwa mchezaji huyo. 

Reina na Barcelona 
Golikipa wa Liverpool Pepe Reina ameonesha nia ya kujiunga na Barcelona baada ya golikipa wa Barcelona kutangaza kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.  Reina aliyasema hayo siku alipokuwa anazindua tovuti yake na kusema “natamani kurudi tena Barcelona siku moja”. Reina kabla ya kujiunga na Liverpool alishachezea Barcelona kwenye kikosi cha kwanza na alihamia Villarreal kabla ya kwenda Anfield. 

Navas na Man city
Man city imetenga kiasi cha paundi mil 30 ili kumsajili mshambuliaji wa Sevilla Jesus Navas licha kupata upinzani mkali kutoka kwa Real Madrid ambao pia wanamhitaji mchezaji huyo. Sevilla wenyewe wapo tayari kumuuza mchezaji huyo kwa Man city kwani wanatarajia kupata pesa nyingi zaidi kuliko kwa Madrid. 

Bale na Real Madrid
Wakala wa Gareth Bale amesema yupo tayari kupokea ofa kutoka kwa Real Madrid ya kumsajili mchezaji huyo ambaye ni ghali kuliko wote sokoni muda huu. Real Madrid wametenga kiasi cha paundi mil 65 ili kumsajili Bale licha ya kuwa klabu ya Tottenham ilishatangaza kuwa mchezaji huyo ana gharimu kuanzia paundi mil 80. Mapema wiki hii rais wa Real Madrid Perez alitangaza nia ya kumsajili mchezaji huyo na kusema wamepatia kazi hiyo Zinedine Zidane ili ahakikishe Bale anasajiliwa na Madrid jambo ambalo wanaamini litafanikiwa. 

Mertinez na Everton
Roberto Martinez leo alikutana na mwenyekiti wa klabu ya Everton Bill Kenwright ili kuongea naye kuhusu kuchukua nafasi ya Moyes aliyekuwa akiifundisha klabu hiyo kabla ya kujiunga na Man utd. Martinez alikuwa ni kocha wa Wigan aliyejiuzulu na ndiye anaonekana kuwa chaguo la kwanza kumrithi Moyes kuifundisha Everton, lakini bado haijawekwa wazi walichokubaliana kwenye mazunguzo yao. 

Cavani na Man city
Kocha mpya wa Napoli Rafa Benitez ameanza kumshawishi mshambuliaji wa klabu hiyo Edinson Cavani ili abaki kwenye klabu hiyo kwa msimu ujao. Cavan alishaonesha nia ya kujiunga na vilabu vya Uingereza Chelsea na Man city na alikuwa kwenye hatua za mwisho kuhamia Man city wiki hii lakini mpango huo umekwama baada ya Benitez kutua Napoli. 

David Villa na Tottenham
Klabu ya Tottenham ipo kwenye maongezi ya mwisho mwisho na klabu ya Barcelona ili kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo David Villa. Tottenham wameomba kumsajili Villa kwa paundi mil 12 ofa ambayo bado inafikiriwa na uongozi wa Barcelona licha ya kuwa Villa mwenyewe amependa kujiunga na Arsenal badala ya Tottenham. 

No comments:

Post a Comment