Wednesday, May 29, 2013

Wachezaji wa Yanga kupewa mil 3.3 kila mmoja

Baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara, klabu ya Yanga inatarajia kuwapa kila mchezaji mil. 3.3 kama zawadi yao kwa kutwaa ubingwa. Kwa mujibu wa Mwananchi ni kwamba fedha zilizotengwa kwa wachezaji ni zile za ubingwa Sh70 milioni kutoka Vodacom, Sh50 milioni (Supersport), Sh80 milioni (klabu) na wadhamini wa klabu hiyo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wanaotoa Sh30 milioni. Hivyo mmoja wa kiongozi wa ndani wa Yanga alihojiwa kuhusiana na mgawanyo wa fedha hizo kwa kila mchezaji na kusema “Siwezi kukwambia wachezaji watakaopata wako wangapi, lakini ninachofahamu wachezaji wote watapata Sh3.3 milioni wakati benchi la ufundi na watu wengine walioisaidia timu kutwaa ubingwa watapata zawadi kwa nafasi zao,”. Mbali na hayo pia alisema wachezaji watapewa fedha hizo mara baada ya kombe la Kagame kumalizika. 

No comments:

Post a Comment