Monday, June 3, 2013

Boban ajiunga Coastal baada ya kutemwa Simba

Mshambuliaji wa Simba Haruna Moshi ‘Boban’ leo amejiunga rasmi na klabu ya Coastal Union ya Tanga kwa mkataba wa mwaka mmoja. Moshi amejiunga na klabu hiyo baada ya kutemwa na klabu ya Simba kwa kile kilichosemwa kuwa kiwango chake kimeshuka, mbali ya Moshi wachezaji wengine saba wametajwa kutemwa na klabu ya Simba na kwasasa wanatafuta klabu za kuchezea kwa msimu ujao. Wachezaji wengine waliotemwa ni Ngalema, Chombo, Nyosso, Sunzu, Maftah, Keita na Abdallah Juma. Klabu ya Simba imefikia uamuzi huu katika jitihada zake za kurudisha hadhi yake baada ya kufanya vibaya kwenye ligi kuu msimu uliopita ambapo ilimaliza ligi kwenye nafasi ya tatu tafauti ya pointi 15 na wapinzani wao wa jadi Yanga ambao ni mabingwa wa ligi kuu mwaka huu. Katika kuimarisha kikosi chake, klabu ya Simba hadi sasa imeshasajili wachezaji wanne ambao ni Ntalla kutoka Kagera sugar, Abel Dhaira kutoka Uganda, Twaha kutoka Coastal Union na Pazi kutoka Azam fc. 

No comments:

Post a Comment