Saturday, June 29, 2013

Brazil wapo tayari kuikabili Hispania kwenye fainali

 photo 1043454627_zps1536c091.jpg
Wachezaji wa Brazil wakipiga vyombo vya muziki wakati wakiwa safarini kutoka Belo Horizonte wakielekea Rio de Janeiro tayari kwa mechi yao ya fainali dhidi ya Hispania. 
 photo 17029000_zps69653520.jpg
Wachezaji wa Brazil wameonekana wenye furaha na imani kubwa ya kushinda mchezo huo na wametoa ahadi ya kuvunja rekodi ya Hispania ya kutokufungwa tokea mwaka 2010. Je furaha zao zitaendelea baada ya mechi au?? jibu kamili ni baada ya mechi kuisha.
 photo 2082448325_zpsf9286058.jpg
David Luiz anatarajia kucheza kwenye mechi ya fainali licha ya kuvunjika mfupa wa pua. Imesemekana baada ya kumaliza michuano hii atafanyiwa matibabu ya uhakika ili kulinda pua yake isiweze kupata majeraha siku za mbeleni
 photo 365599421_zpsa91c5d70.jpg
Neymar anatarajiwa kuendelea kuonesha umahiri wake kiwanjani akiwa ni moja ya wachezaji walionesha kiwango kizuri kwenye michuano hii hadi sasa. Neymar ataingia uwanjani akijua fika macho ya watu wengi yatakuwa yakimuangalia yeye hususani Wahispania na wadau wa Madrid na Barcelona ili kutathimini vyema uwezo wake, hivyo atajitahidi kufanya kila awezavyo aweze kung'ara kwenye mchezo huo.  
Mercelo anaonekana akiwa hana wasiwasi wowote wa mechi, kwani wachezaji wengi wa Hispania ameshazoea kucheza nao, hivyo mazingira ya mechi hii kwake sio mageni sana. 

No comments:

Post a Comment