Friday, June 28, 2013

Everton waibania Man utd kumsajili Leighton Baines

Klabu ya Everton, imekata ombi lililowasilishwa na Manchester United la kutaka kumsajili beki wa kushoto Leighton Baines kwa kitita cha paundi mil 12. Kocha mpya wa Manchester David Moyes ambaye alisajiliwa Everton alitaka kumasjili mchezaji huyo ili kuimarisha safu yake ya ulinzi upande wa kushoto na kupunguza utegemezi wa Patrice Evra (32) ambaye umri wake umekwenda. Everton wamegoma kumuuza mchezaji huyo kwa madai kuwa sio mchezaji wa kuuzwa, lakini ripoti zinasema klabu ya Manchester United inajianda kuwasilisha ombi lingine baada ya kuongeza fedha za kumsajili. Kwa kawaida, makocha wengi wanapohama huwa wana kawaida ya kuhama na mchezaji/wachezaji wazuri kutoka kwenye klabu waliyokuwepo, matarajio haya pia yanatarajiwa kwa David Moyes, na hadi sasa Fellaini na Baines ndiyo waliotajwa kuhamia Man utd na mazungumzo bado yanaendelea.  

No comments:

Post a Comment